Diamond Platnumz awaandikia barua wasanii wanaokosoa nyimbo zake
Diamond Platnumz hivi karibuni aliwaandikia wasanii wenzake barua huku akiwasihi wanapoandika nyimbo zao lazima wawe na malengo ya kuwafikia watu wengi na sio watanzania peke yao.
Kupitia mtandao wake wa Instagram Diamond aliandika huku akitoa mfano wa muziki wake. Kulingana na alichaondika Diamond Platnumz alisema kuwa muziki wake umemfungulia njia za kupiga show nchini ambazo yeye hakuwa anajua anaweza kufika.
Mkali huyu wa bongo aliandika kusema
Leo ningependa nitoe ujumbe huu kwa wasanii wenzangu pendwa… Siku hizi mjini kila mtu anajifanya yeye soko la Muziki analijua sana na bingwa wa kuelekeza na kukosoa nyimbo za watu….Pasipo kujua kuwa kila nyimbo ina soko lake na kila mwanamuziki anapotoa nyimbo anakuwa na malengo ama plan ambayo ameidhamiria…leo ntakupostia baadhi ya nyimbo ambazo wakati nazitoa zilidharauliwa, zilipingwa sana na wanaojifanya wajuaji wa Muziki… pasipo kujua kuwa dhamira ama nini yalikuwa malengo yangu….kwakuwa nilikuwa na imani na kufahamu nikifanyacho basi nikawa nawaekea tu neno #MALENGO na leo hii nyimbo hizo ndio sababu kubwa ya mimi kuwa na Show za nchi ambazo kiukweli sijawai tegemea fika na kufanya show za Uwanjani….. sababu yangu kubwa leo ni kuwasihi wasanii wenzangu kuwa mnapokuwa na kitu ambacho mnamalengo ama target nacho msiogope kukisimamia…lakini pia kuwajuza kuwa kila kanda ina maadhi ya muziki wake ambao unaupenda, hivyo ukitaka kufanikiwa kushika kanda zote usiogope kufanya Muziki tofautitofauti ili kuongeza Mashabiki ila ukiogopa kufanya muziki wa mahadhi flani kisa wabongo wataongea na kuamua tu kutoa kina “UKIMUONA” Basi hatutafanikiwa kuteka Masoko na chi zingine… #SimbaInZambia