Diamond Ndani ya Billboard kwa Kishindo.
Msanii Diamond Platinumz amekuwa ni moja ya mastaa ambao ndoto zao zinaanza kutimia kwa kuandikwa katika makala za mtandao wa billboard nchini.katika makala hiyo Diamond amewekwa katika picha ya pamoja na mstaa wengine wanne akiwepo Wizkid, Tiwa savage na Davido.
Katika makala hiyo inaonyesha ni jinsi gani muziki wa Afrika unavyojitahdi kumtafuta star wa pop Dunianai kutoka afrika pia.Hii imekuja baada ya kampuni kubwa ya muziki Duniani Universal Group ambayo pia inasimamia kazi za Diamond kwa sasa kupitia tawi lake la nchini uhalanzi ilitangaza kununua hisa za asilimia 70% za lebo ya AI records za nchini kenya.
UMG itakuwa inafanya kazi ya kusambaza kazi mbalimbal za wasanii kutokea AI Records Duniani kote ikiwepo kwenye mitandao mikubwa tofauti tofauti Duniani.