Diamond Avunja Ukimya Mimba ya Tunda

Msanii mkubwa wa bongo fleva ambae kila siku haishi na drama za kubadilisha wanawake kama ambavyo mitandao imekuwa ikimnasa Diamond Platinumz amefunguka na kuongelea mahusiano yake na video vixen mkali bongo Tunda.

Katika usiku wa kutambulisha msanii mpya katika kundi lao la WCB, uliofanyika katika ukumbi wa Hyatt Regency jijini Dar, Diamond amesema kuwa hakuna ukweli wowote juu ya maneno ya watu na hana uhusiano wowte na Tunda kama watu wanavyodai.

download latest music    

Huku akionekana  na sura ya furaha Diamond amesema kuwa akishangaa kila mwanamke mzuri amekuwa akitoka nae yeye , kwanini mitandao wamekuwa hawaachi kufatilia mambo hayo.”kwanini kila mwanamke mzuri nakuwa natoka nae mimi tu au mimi nina asali,sina mahusiano na Tunda” alisema Diamond Platinumz huku akicheka kwa dharau na kuondoka.

Hata hivyo siku hiyo wa uvumbuzi wa nyimbo mpya ya Maromboso Diamond aliweza kumualika pia Wema Sepetu ,mwanamke ambae alishawahi kuwa nae katika mahusiano kipindi cha nyuma  na kuachana nae baadae na hata kuingia katika bif zito, ambapo uwepo wa mwanadada huyo ulizua gumzo kubwa na kufanya watu waamini kuwa wawili hao wamerudiana hasa katika kipindi hiki ambacho Diamond yupo katika mgogoro na mzazi mwenzie Zari.

Alipoulizwa kuhusu kumualika Wema Sepetu, Diamond alijibu kuwa maswala ya kugombana yalishapita na wakati , kipindi hicho walikuwa wadogo laini sasa hivi wamekuwa kwaio wameacha utoto”sasa hivi tumekuwa kwaio yale ya bifu yalikuwa ni utoto  tukiendelea kugombana ina mana tunamindiana, na hata tukitoka hapa tunaenda maisha basement, madam ni rafiki yangu sana na hata mwaliko huu nilimpigia nikamwambaia madam usikose nakuomba sana sana.”

Alipoulizwa kuhusu kutokuwepo kwa Hamisa katika party hiyo Diamond alijibu kuwa alitoa mwaliko kwa kila mtu na kama Hamisa hakuwepo basi labda hakupata mwaliko kwa muda au hawakumkuta ,lakini yeye amemwamlika kila mtu hata Tunda amekuja.”Hamisa alipelekewa kadi lakini labda alikuwa hayupo, nimemwalika kila mtu.Hata Tunda yupo”  Alisema Diamond huku akinyoosha mkono kumsalimia Tunda na kumuita.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.