Diamond Atoa Siri, Aelezea Sababu ya Wasanii wa WCB Kufanikiwa.
Msanii mkubwa bongo Diamond Platinumz aefunguka na kutoa siri ya kinachowafanya wasanii wote katika lebel yao ya Wcb kuwa wanafanikiwa kila wanapotoa wimbo unapendwa na hata kama imechukua muda mchache kuja katika game la muziki.
Diamond amefunguka hayo siku ya Jumamosi alipokuwa akimkaribisha na kumtambulisha msanii mpya wa wcb , maromboso ambae mara ya kwanza laikuwa ktaika kundi la Ya Moto Band kabla kundi hilo halijavunjika na kusambaratika.
Diamond anasema kuwa katika kuwatoa wasanii wake katika lebel hiyo hajawahi kufanya hivyo kama biashara kama wanavyofanya wengine bali yeye anawato wasanii wengine kwa sababu anataka watoke na waweze kusaidiana kwa sababu wapo wengi wana vipaji lakini wanashindwa kutoka.
Diamond anaongezea na kusema kuwa kinachomtia moyo kutoka kwa wasanii hao ni kwa sababu wamekuwa wakijituma sana na hata kuacha kulala usiku ili kuhakiisha kuwa kazi zao zianakwenda vizuri kwa sababu hawafanyi kwa ajili yake bali ni kwa ajili yao na familia zao.
nafikiri kwa sababu mimi sifanya hivyo kibiashara, watu wengi wamekuwa wakiifanya kibiashara lakini mimi ninafanya kwa ajili ya kujikomboa,na kila mtu apate kulingana na kazi ile anayoifanya.na ndio maana kila mtu anaefanya kazi wcb anafanya kazi kwa kujituma na kwa moyo mmoja kwa sababu anajua kabisa kile anachokitengeneza hamtengenezei Diamond au Wcb, bali anafanya kwa ajili ya yake na familia yake.
Diamond ni msanii aliyejitolea kwa muda mrefu sasa kutoa wasanii wadogo na kuwaingiza katika game la muziki, na kwa bahati nzuir wasanii wote kutoka katika lebel hiyo wamekuwa wasanii wakubwa na kufanikiwa sana hata kuanza kutambulika kimataifa,wasanii kama Harmonize, Rayvanny, Lavalava na Queen Darlen ni wasanii zao kutoka Wcb na wamekuwa wakifanya vizuri ndani na nje ya Tanzania.