Diamond Athibitisha Kuzama Kwenye Penzi Zito na Tanasha
Staa wa muziki wa Bongo fleva na CEO wa WCB Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz amethibitisha kuwa amezama vibaya kwenye Penzi na Mpenzi Wake Mpya Tanasha Donna Oketh.
Diamond alitangaza kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na mrembo kutoka Kenya Tanasha ambaye ni video vixen na Mtangazaji wa redio.
Lakini pamoja na kuwa pamoja kwa muda mfupi tu Diamond ameweka wazi ni Jinsi gani anavyomzimia mrembo huyo kwani amekuwa akimuanika kwenye mtandao wa kijamii.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond Platnumz ameweka video yake na Tanasha inayomuonyesha akimtengeneza nywele Mpenzi Wake huyo na kuweka wazi Jinsi anavyomzimia.
Basi na Mie nikiingiaga kwenye mapenzi nazama mzima mzima kama boya….Matokeo yake nikizinguliwa naanza kutoa Povu…”.
https://www.instagram.com/p/BrsWX0MFzNh/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1t7cbpa4u9y9e