Diamond Atangaza Kumuoa Mrembo Kutoka Kenya
Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka WCB Diamond Platnumz ametangaza kufunga ndoa na mrembo ambaye ni mwanamitindo kutoka Kenya Anayejulikana Kama Tanasha Donna Barbier.
Diamond ametangaza ndoa na mrembo huyo Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa ambapo Alikiri kuwa kwenye mahusiano na mrembo huyo ambaye ni mtangazaji wa Radio NRG ya jijini Mombasa nchini Kenya.
Diamond alisema kuwa, mara baada ya kuachana na mzazi mwenzake ambaye alizaa naye watoto wawili, Princess Tiffah na Prince Nillan, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, wasichana wengi ‘aliowatokea’ na hata Zari mwenyewe hawakulichukulia jambo la ndoa kwa uzito kama alivyofanya Tanasha.
Tanasha ndiye mwanamke pekee aliyeonesha kujali na uzito juu ya jambo hilo hivyo rasmi natangaza kumuoa huyu.
Lakini nimejiridhisha kwamba mbali na umbo na mvuto wa kipekee pia ni mwanamke mwenye tabia nzuri.”
Alipoulizwa juu ya uwepo wa Tanasha kwenye ufunguzi wa Tamasha la Wasafi Festival mjini Mtwara, Diamond alifunguka kuwa ni kweli alikuwepo, lakini watu wengi hawakumjua kutokana na usiri uliokuwepo wa kumuonesha kabla ya yeye mwenyewe kumtambulisha alipokuwa stejini.
Nitakuwa na shoo kesho nchini Kenya katika Mji wa Thika ambapo Tanasha atanitambulisha rasmi kwa wakwe zangu“.
Diamond amesisitiza kuwa Tanasha ndiye mwanamke pekee ambaye amejikuta kweli ana vigezo vyote vya kuwa mke wake pamoja nakwamba siku za Nyumba alishawahi kutangaza ndoa na maex zake kama Zari, Wema, Penny na Jokate.