Diamond Ataja Project Anayoipenda Zaidi Kufanya.
Inawezekana hiki ndicho alichokuwa anataka kukifanya muda wote lakini muda ulikuwa bado haujaruhusu na baadhi ya mambo yalikuwa bado hayajakaa sawa kwake,Diamond amekuwa akisema kila siku kuwa anapenda sana kusaidia wengine kwa kuwa anaamini kuwa hata yeye amepitia magumu sana mpaka kuwa yeye kama yeye.
Diamond anaamini kuwa wapo vijana wengi mitaani wamekuwa wakiangaika sana kuendelea na kuvitambulisha vipaji vyao kama ndio njia ya kujipatia vipato lakini inakuwa kazi kwa sabau wanakosa mtu wa kuwavuta pale walipo.
Katika ukurasa wake w Instagram Diamond aliweka wazi kitu anapenda kufanya ni project yake mpya ambayo inaanza sasa ya kuwa na media yake mwenyewe, kwa kuwa anaamini kuwa atawafikia vijana wengi sana na kuwainua wengi kutoka pale walipo.
they asked me, what have been my favorire project of all that have done…i said..NEXT ONE!!…wananiuliza ni project ipi ninayoipenda zaidi katika zote nilizowahi kuzifanya ….nawaambia ni hii inayofuata ..maana naijua haswa na niliingojea kwa hamu …na itaniwezesha kuwanyanyua na kubadilisha maisha ya vijana wengi mtaani.-Alithibitisha Diamond katika ukurasa wake wa Instagram.