Diamond Aongelea Swala la Rick Ross Kufuta kwa Picha Zake
Msanii mkubwa bongo Diamond Platinumz amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu swala la msanii mkubwa duniani kufuta picha zake katika ukurasa wake wa instagram na kuacha picha ya mwanadada Huddah Monroe.
Diamond anasema kuwa ukurasa wa instagram ni wa mtu binafis hivyo nakuwa na maamuzi yake ya matumizi katika ukurasa huo.Diamond anasema kuwa hata yeye amekuwa akifuta picha za watu mbalimbali kama tukio alilokuwa ameripost limeisha hivyo kuweka na kufuta picha ya mtu ni kiyu cha kawaida.
Hata mimi hiyo ni tabia yangu, ninaweza kukupost kama ni birthday yako alafu baadae nafuta kama birthday yako imepita nakutoa.sasa kama birthday likuwa jana na leo unataka tena.
Anasema kuwa watu wengi wamekuwa wakiweka picha na kuto akutokana na wigi wa matukio kwa sababu ya kuweka matukio ya mbele, lakini pia diamond amekanusha tetesi za kuwa msaniii huyo mkubwa alikataa kutoa nae video ya wimbo wa waka waka, Diamond amesema kuwa rick ross alikuwa na wasanii wengi kwaio aliwapa muda mchache tu wa kutengeneza video.