Diamond Amliza Nisha Bebe.
Msanii wa muziki nchini Diamond Platinumz amemtoa machozi mwanadada Nisha baada ya kusikiliza wimbo wak wa sikomi.
Nisha amepost video katika ukurasa wake wa instagram akiwa anasikiliza wimbo wa Sikomi huku akitoa machozi kama ambavyo wimbo huo umekuwa ukitoa maudhui ya majonzi kwa mtu aliyeumizwa na mapenzi.
Nisha ni moja ya wasanii wa kike ambao mara nyingi wamekuwa wakilalamika sana kuuumizwa na mapenzi tena kwa kukimbiwa na wapenzi wao na kwenda kutoka na watu wengine.
Hivi karibuni , Nisha aliingia katika mgogoro na Snura baada ya kusemekana kuwa Snura alimuibia aliyekuwa mpenzi wake nisha kwa makusudi huku akijua kabisa kuwa ni mpenzi wa Nisha.