Diamond Amefunguka Kuhusu Mahusiano Yake na Baba Yake

Staa wa muziki wa Bongo fleva Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz ‘ Amefunguka kuhusu uhusiano aliokuwa nao na baba yake mzazi.

Sio siri kuwa Diamond na Baba yake mzazi anayejulikana kwa jina la Mzee Abdul Juma hawa na uhusiano mzuri sana. Mara kwa mara Baba Diamond amekuwa akilalamika kwenye vyombo vya habari kuwa hayupo kwenye maisha ya mwanaye kumaanisha hata wajukuu zake hajawahi kuwaona.

download latest music    

Diamond aliwahi kuwa muwazi na kusema kuwa hajalelewa na Baba yake na kusema Baba yake aliokuwa cha wakati mdogo sana na yeye alilelewa na mama yake. Lakini siyo hayo tu pamoja na Diamond kuonekana supastaa na kuishi maisha fulani ya kifahari ni tofauti na maisha anayoishi baba yake.

Kwenye mahojiano aliyofanya jana akiwa anatoka mahakamani kufuatia kesi yake na mzazi mwenzake Hamisa, Diamond alisema mambo kama hayo yanaweza kuharibu mahusiano yaliyopo kati ya Baba na mtoto kwani huwezi kujua akikua ataambiwa nini kuhusu Baba yake.

Diamond alifunguka haya kuhusu uhusiano alionao na baba yake kwa hivi sasa:

Nimejifunza kwamba sio kila mtoto ambaye haishi na mama yake au na baba yake basi ana tatizo naye hili suala langu na mwanangu limenifunza kitu kuhusu uhusiano wangu na baba yangu ingawa sasahivi tupo sehemu nzuri nawasiliana naye vizuri na kwenye kusaidia basi namsaidia na nikiwa Sina uwezo basi namwambia sina uwezo lakini kwa bahati mbaya hatukubahatika kuwa na mahusiano ya karibu kama nilivyo na mama yangu na hiyo inaniwia ugumu kwa sababu sijamzoea kihivyo ndio maana hunioni naye kila sehemu kama mama yangu”.

Lakini pia Diamond amewaomba waandishi wa habari waache tabia ya kuchonganisha familia yake na kuongelea kitendo cha mwandishi kumpeleka baba yake nje ya geti la nyumba yake na kuandika kuwa Diamond kakataa kumfungulia mlango baba yake kitendo alichosema hakipendezi hata kidogo.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.