Diamond Aiangukia BASATA Aomba Japo Kuperfom ‘Mwanza’ Stejini
Msanii wa muziki wa Bongo fleva na CEO wa WCB Diamond Platnumz ameibuka na kuiomba ruhusa Baraza la Sanaa kutumia wimbo wake walioufungia wa Mwanza kuperfom stejini.
Wiki chache zilizopita wimbo wa ‘Mwanza’ ulitoka lakini mara moja BASATA waliufungia wimbo huo kwa madai ya kukiuka maadili ya Kitanzania kwa kubeba ujumbe wenye lugha ya matusi.
Lakini Diamond Platnumz amefunguka na kuwaomba Basata kuutumia wimbo wao ba Rayvanny wa Mwanza kwenye tamasha lao la Wasafi Festival 2018.
Kupitia ukurusa wake wa Instagram Diamond ameandika hayo.