Daz Baba Aongelea Machungu Yake Ya Kuvunjika Kwa Daz Nunda
Likiwa kama moja ya makundi kongwe kabisa ya mzuki nchini , kundi la Daz Nunda lilikuwa likifanya vizuri sana likiundwa na wasanii kama Daz Baba, Daz Mwalimu na Ferooz ambao walitoa nyimbo nyingi ikiwepo kamanda wimbo ambao ulikuwa ukitamba sana kipindi icho .Lakini kundi ilo lilikuja kuvunjika na watu wote kusambaratika huku haijulikani mchawi nani.
Akiongea na eNews ya Clouds Tv, mmoja wa wasanii waliokuwa wakiunda kundi ilo aliongea kwa machungu kabisa kuhusu kuvunjika kwa kundi ilo kulivyomuumiza ingawa anasema hakuna alichojutia sana baaada ya kuvunjika kwa kundi ilo.
“Sina ninachokijutia zaid ya kuumia baada ya kuvunjika kwa kundi la Daz Nunda,kuna ile moment mtu amekuja tu akasema bana Daz Nunda wako ile tena,ilimradi tu yeye apate kitu,wakati huku Daz Nunda upendo ukafa .” aliongea Daz Baba
Hata hivyo Daz Baba anasema kuwa kuna kipindi walianzisha kundi jingine lakini bado haikuwa kama Daz Nunda kwa sababu muda wote wanapofanya kazi wanakuwa wanatamani sana ingekuwa Daz Nunda ndo ingekuwa inafanya hivyo lakini basi ule upendo ukawa umeshavunjika tayari.
Hata hivyo Daz Baba anafunguka kuwa kwa sasa ambapo amekuwa kimya kwa muda mrefu sana , amekuwa akifanya kazi zake za muziki ktika matamasha na show mbalombali nchini uganda na kenya, lakini pia amekuwa akifanya biashara za kuuza ma-tshirts, top za kike na stickars za magari kwa mashabiki wake kutoakana na brand yake ya daz baba , pamoja na ile ya umbo namaba naen kwa wakina dada.
Akiwa mmoja wa wasanii waliokuwa wakifanya vizuri katika kundi Daz Baba alikuwa hitmaker wa nyimbo kama Umbo namba nane na wimbo wa Wife ambao ulikuwa ukiimbwa katribia na kila rika.Hata hivyo baada ya kuvunjika kwa kundi ilo kulikuwa na tetesi nyingi zilikuwa zikitawala kuw wasanii wa kundi ilo wameanza kutumia unga na vitu kama hivyo huku msanii mwenzao Ferooz akionekana kuharibikwa zaidi.
Daz Baba anasema ndoto za maisha yake zilikatika pale ambapo baba yake mzazi alipouwawa na watu wasiojulikana ivyo yeye akashindwa kuendeelea na masomo yake ya uinjinia ambapo alitakiwa kwenda kusomea nje ya nchi.
Wasanii walikuwa wakiunda kundi la Daz Nunda.Ferooz na Daz Baba