Dayna Nyange Awachana Wasanii Wa Kike
Msanii wa muziki wa Bongo fleva nchini Dayna Nyange amewajia juu wasanii wa kike wanaoingia kwenye tasnia ya Bongo fleva bila ya kuwa na kipaji chochote.
Dayna amewataka wasanii hao watambue kuwa kama kazi zao hazitakuwa nzuri lazima zitafeli, licha ya pesa nyingi walizotumia kuwekeza katika harakati za kuingia kwenye Sanaa hiyo.
Kama kitu kizuri kitabaki, na kama kitu kibaya kitapotea, wengi wanaotumia pesa huwa wanatumia wakiamini watawapiku watu fulani kuwa watu fulani, lakini kazi kama sio nzuri haijiuzi unakuja kujikuta unaongeza tu mtaji, wengine wakiwa na nia na wakajifunza watabaki”.
Lakini pia Pia Dayna amewataka wasanii hao kuchukua muda kujifunza au kuomba msaada kwa wanaojua, ili kuweza kujitengeneza zaidi na wasipoteze pesa zao ambazo hazitarudi kutokana na kazi hizo.
Hivi karibuni mwanamitindo, Hamisa Mobetto kwa mara ya kwanza ameachia nyimbo zake mbili zinazojulikana kama ‘Madam Hero’ na ‘Tunaendana’ akifuatiwa na mwanadada mwingine maarufu katika mitandao ya kijamii, Irene Louis maarufu ‘officiallyyn’ ambaye ameachia nyimbo inayojulikana kwa jina la ‘Chafu’.