Davina Ataja Sababu Za Kuolewa Baada Ya Ndoa Yake Kuvunjika
Msanii mkongwe wa Bongo movie Halima yahaya maarufu kama Davina amefunguka na kutangaza kuwa ana mpango wa Kuolewa Tena hata baada ya kila kiapo cha kutofanya hivyo.
Davina ambaye aliyewahi kuolewa siku za nyuma na ndoa yake kuvunjika ambapo alisema hatakuja Kuolewa Tena amejikuta akisahau kiapo chake na kutangaza Tena ndoa.
Katika Interview yake aliyofanya na Global Publishers, Davina amesema kuwa ni kweli aliwahi kusema kwamba hana mpango wa kuingia tena kwenye ndoa, lakini kwa kuwa ni binadamu kwa sasa wakati umefika na tayari ana mchumba ambaye anatarajia kuingia naye kwenye ndoa mwakani.
Ikiwa mimi ni binadamu niliyekamilika, siwezi kukaa hivi bila kuolewa tena milele, niliyoyasema mwanzo ni maneno tu, lakini kwa sasa tayari nina mchumba na Mungu akipenda nitaingia tena kwenye ndoa mwaka ujao“.