Davina Akiolewa Tena Naandamana:-Mayasa
mwanadada kutoka bongo movie Mayasa Mrisho amewashangaza watu baada ya kusema kuwa rafiki yake kipenzi davina akiolewa basi yeye ataandamana kwa sababu davina ameshazaa watoto watatu huku wakiwa wa baba tofauti na wanaume hao wamekuwa wakimuumiza sana kiasi kwamba amekuwa na machungu sana na kuumizwa na mapenzi .
Mayasa anasema kuwa wa upand wa rafiki yake huyo Davina ameshaona kuwa hakuna haja tena ya kuendelea kuwaza maswala ya ndoa au mapenzi kwa sasa anwaza sana maswala ya pesa kwa ajili ya kuweza kuwalea watoto wake.
Yaani siku Davina akiolewa tena naandamana kwa maana wanuame wamemtenda sana jamani,sasa hivi ni muda wa kutafuta pesa tu kwa ajili ya kufanya mabo mbalimbali ya kimaisha kama anavyofanya ili aweze kuwalea watoto wake.
Hata alipoulizwa Davina mwenyewe alisema kuwa kwa sasa hana mpango wa ndoa tena zaidi ya kutafuta ela kwa ajili ya kulea watoto wake na ndio maana amekuwa akisafiri nje ya nchi ili kuweza kufanya baishara zake.