Davina Akanusha Tetesi za Kutumia Madawa.

Wasanii wengi bongo wamekuwa wakiusishwa sana na uuzaji na utumiaji wa madawa ya kulevya , hii inawezekana labda kutokana na hali ya sanaa ilivyo nchini kiasi kwamba mtu anaona kuliko kusota muda mrefu katika kazi zake ili kufanikiwa na kupata kipato chao wanaona ni bora kutumia njia rahisi ya kuuza madawa ili kuwa mabosi.

Msanii wa bongo movies mwanadada Davina , amekanusha tetesi za kufanya biashara ya unga  hasa anapokuwa nasafiri kwenda duabai ambapo kwa hivi karibuni amekuwa akisafiri sana kwenda huko na kuweka picha katika mitandao , lakini kitu cha ajabu watu wamekuwa wakimtuhumu kuwa anaposafiri kwenda huko amekuwa akisafirisha unga.

download latest music    

Davina anasema kuwa safari zake a kwenda dubai sio za kusafirisha unga ila amekuwa akifanya baishara halali kabisa ambayo inamuingizia kipato kwa muda mrefu na wala sio vinginevyo.

Yaani mimi safari zangu ni kwa ajili ya baishara zangu tu na wala sio vinginevyo, kuhusu kujihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya mimi huwa nasikia kwenye radio tu  na magazeti wala sithubutu kabisa maana maisha bado nayapenda.-Alisema Davina aliyekuwa akiongea na Amani kwa njia ya simu.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.