Daktari maarufu Bongo adai kuwa Wolper ni ‘Wife material’

Japo Wolper bado hajapata mtu ambaye anaweza kumuoa mrembo huyu wa muvi za bongo sasa hivi anatoka na mwanaume ambaye anasemekana ni mdogo kumshinda.

Hii iliwafanya watu wengi kumchana lakini Daktari mmoja kutoka Bongo, Dk Fadhili Emily ameonekana kuwa na maoni tofauti. Akizungumza katika mahojiano alisema kuwa mrembo huyu akona uwezo wa kuwa mke mzuri kwam tu yeyote.

download latest music    

“Nimeona kwenye mitandao, wanamuandama kuwa hajatulia na kwamba ana msururu mkubwa wa wanaume ambao ametembea nao, kimsingi huyu mrembo hajapata tu mtu sahihi lakini anafaa kuwa mke wa kulea familia kabisa,”

Hata hivyo daktari huyu pia anasemekana kuwa hapo awali alitoka kimapenzi na Wolper lakini wakamwagana kwa sababu ambazo sio wengi wanajua.

 

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua