Cyril Kamikaze Adai Mapenzi Yake na Feza Hayaeleweki

Mwanamuziki wa Bongo fleva Cyril Kamikaze ameibuka na kudai kuwa uhusiano wake na mwanamuziki mwenzake Feza Kessy ni mgumu kuelewa yaani its ‘complicated’.

Wiki chache zilizopita msanii Cyril alikiri kuwa yeye na Feza wana uhusiano wa kimapenzi baada ya kukataa kwa muda mrefu walipokuwa wanaulizwa huku wakidai kuwa walikuwa marafiki wa kawaida na kukana mahusiano yoyote ya kimapenzi.

download latest music    

Lakini katika hali ya kushangaza wiki chache baada ya kukiri kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Feza na kuweka wazi kuwa Feza ndiye mwanamke anayempenda kwa sasa, Cyril ameibuka na kudai kuwa yeye na Feza hawana uhusiano huo tena bali chochote walichokuwa nacho hakieleweki.

Wiki iliyopita Feza alifanya mahojiano na kituo kimoja cha redio na kukiri kuwa anampenda sana Cyril licha ya kwamba Cyril amekuwa hataki kulikubali hilo na kuweka wazi uhusiano wao.

Baada ya utata huo, Millard Ayo Tv ilimtafuta Cyril ili atatue utata huo uliopo juu ya uhusiano wake na Feza na alifunguka yafuatayo;

Ninaweza nikasema uhusiano wangu na Feza upo complicated unajua nilifanya mahojiano na moja ya media ikabidi nikubali kwa sababu nadhani muda ulikuwa unaenda sana na kwa wakati huo nilikuwa natakiwa niitambulishe kazi yangu, lakini mahusiano yetu yapo complicated sana lakini nadhani muda ukifika kila kitu kitakuwa sawa alafu isitoshe mimi sio mtu ambaye ninaweza kuweka hisia zangu wazi ili tu nifurahishe watu wengine haya ni mambo ambayo mimi na Feza tutatakiwa tukae ili tuweze kuweka sawa lakini kuna changamoto kwenye mahusiano yoyote”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.