Chuchu Hansy Amefungukia Tetesi Za Ray Kuwa Tasa
Muigizaji wa Bongo movie Chuchu Hansy amefungukia tetesi zilizowahi kusambaa mitandaoni kuwa mpenzi wake staa na mkongwe wa Bongo movie Ray Vincent Kigosi ni tasa.
Chuchu na Ray wamekuwa na uhusiano wa kimapenzi kwa miaka mingi sasa na kwa pamoja wamezaa mtoto mmoja anayeitwa Jayden. Wakati Jayden amezaliwa maneno Mengi yalizuka mtandaoni kuwa Ray anaweza kuwa sio baba mtoto kwa sababu mtoto alionekana kuwa mweupe sana na kuhisi Ray amebambikiwa
Lakini pia watu wengi walidai kuwa Ray sio baba wa mtoto yule kwa sababu kwa miaka mingi amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na wasanii wenzake wawili ambao ni Johari na Mainda lakini hakuna hata mmoja aliyebeba ujauzito wa Ray halo iliyowapelekea wengi kufikiri labda atakuwa hana uwezo wa kuzaa.
Ray aliwafunga mdomo watu wote waliokuwa wanamzushia kuwa ni tasa wiki iliyopita baada ya kuanika picha za Jayden ambaye hivi sasa amefanana naye copy right. Lakini pia Chuchu amefunguka na kuwafunga midomo wote waliosambaza habari hizo kiwa Ray ni tasa.
Kwenye mahojiano na Enews ya East Africa TV, Chuchu Hansy amefunguka yafuatayo kuhusu suala hilo :
Mimi ndio mama wa motto kwaiyo nilikuwa naujua ukwell kuhusu nani baba wa motto lakini sikuona sababu ya kuwajibu kuwa Ray sio tasa nilijua kila kitu kitakuja kwawakati wake na wao watajua alafu wao wanaongea sio Miungu watu anayejua mtu ni tasa ni Mwenyezi Mungu tu”.
Lakini pia Chuchu amekana tetesi zote zilizodai kuwa yeye na Ray wameachana Kisa tu wameacha kuwekana kwenye mitandao ya kijamii bali amesema hawapendi sana kuanika mambo yao kwenye mitandao ya kijamii panini bado wapo wote na wanapendana na wanataka kuongeza mtoto mwingine Mungu akiwaajalia.