Chuchu Hansy Afungukia Habari Za Mimba Yake Kuharibika
Msanii wa Bongo movie na mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva Ray Vicent Kigosi, Chuchu Hansy amefunguka na kuongelea suala lake la mimba kuharibika.
Siku za hivi Karibuni Kumekuwa na tetesi kuwa Mrembo huyo Chuchu Hansy amekuwa katika kipindi kigumu mara baada ya mimba aliyokuwa amebeba kuchoropoka.
Chuchu Hans ametoa povu baada ya kudaiwa kuwa alinasa ujauzito ukachoropoka akiwa nchini Afrika Kusini alipokuwa na Ray kwa ajili ya matembezi ya kifamilia.
Kwenye mahojiano aliyofanya na gazeti la Ijumaa Wikienda, Chuchu alisema anawashangaa wanaomfuatilia kila kukicha. Alisema ni ajabu kuona watu wanamfuatilia kama ana mimba au la.
Kila kukicha watu wanapenda kufuatilia mambo yangu na sijui ni kwa nini maana hata kama nikizaa watoto kumi na Ray, ni sawa kwa sababu ni mwanaume na ananipenda na kujali, kwa hiyo hata kama imetoka nitabeba tena hivi karibuni“.
Ray na Chuchu Hansy tayari wana mtoto mmoja wa kiume anayeitwa Jaden.