“Chiddi Ameletwa na Mungu ‘Special’ Kwaajili Yangu”- Shamsa Ford
Msanii wa filamu za Bongo movie mwanadada shamsa Ford ameibuka na kudai anampenda sana mumewe huyo na anaamini ameletwa maalumu kwa ajili yake.
Lakini pia Shamsa amedai kuwa anaamini kama bila kumuweka ndani huenda hadi leo angekuwa amedoda kwa kitoolewa kwani kwenye ulimwengu huu haoni kama kuna mwanaume aliyestahili kuwa mumewe.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Shamsa alisema kuna sababu nyingi za kumfanya aseme hivyo kubwa ikiwa ni jinsi mwanaume huyo anavyompenda kwa dhati kiasi kwamba anaamini ameletwa na Mungu spesho kwa ajili yake.
Hata kama dunia ingeisha leo na tukarudi mara ya pili mimi bado ningemchagua mume wangu Chid kwa sababu naona ndiye mwanaume pekee aliyekuja kwa ajili yangu. Ananipa furaha isiyo kifani kiasi kwamba naamini kama asingetokea yeye, mpaka leo ningekuwa sijaolewa, yaani ningekuwa bado nasubiri aje hata angechelewa vipi”.