Chid Benz:Mashabiki Wanaosema Nimewachosha Hao Sio Mashabiki Wangu.
Chidi benz kwa sasa yupo uraiani tangu alipokuwa amekamatwa tena mkoani Dodoma kwa tuhuma za kukutwa na madawa ya kulevya na kukaa rumande kwa siku 40 na kuachiwa huku kesi hiyo ikiwa bado haijaisha na kusemekana kuwa wanafatilia swala la upelelezi wa kesi hiyo.
Hata hivyo Chid Benz amefunguka na kusema kuwa watu wengi katika mitandao ambao wamekuwa wanasema kuwa wao ni mashabiki wake, na wamekuwa wakisema kuwa wamechoshwa kusikia na habari zake za madawa ya kulevya kila siku lakini kwa upande wake anaamini kuwa shabiki wa kweli hawezi kumchoka msanii wake zaidi ya kumpa maneno ya kumfariji tu na kama wapo hivyo hao sio mashabiki wake.
Haijalishi Chid anaua anachinja au anafanya nini lakini unapaswa kupenda muziki wake, sometimes unasikia eti tumechoshwa na habari zake kila siku laki i ukweli ni kwamba hao ni mashabiki wa wasanii wengine wala sio mashabiki wangu maana mashabiki wangu wasingechoka.
Akiongelea swala la kumalizika kwa kesi yake , Chid anasema kuwa kwa sasa bado kuna uchunguzi uaendelea lakini wanachoshukuru Mungu ni kwamba pamelegea sio kama pale ambapo walipokuwa mwanzoni.
Hata kama uchunguzi utakamilika na tukakutwa hatuna hatia basi tutashukuru mungu tu lakini hatuwezi kuishitaki serikali kwa sababu no one trust you chid, kwaio tunakaa tunasubiri tu tunaamini kuwa yataisha.
Lakini pia akitoa neno lake kuhusu kufungiwa kwa Nay wa Mitego, Chid Benz anasema kuwa Nay wa Mitego inabidi anabilishe mfumo wake wa kuandika mashairi kwa sababu itafika sehemu watamkariri na kila kosa atakuwa anapewa yeye hata kama nyimbo zake zina mashairi mazuri.