Chemical Asema, Rosa Ree Hayupo Kwenye Anga Zake,Hasifananishwe Nae.

Msanii anaetamba na nyimbo za ku-rap nchini mwanadada Chemical amekataa kufananishwa na mtu yoyote hata kama  ni Rosa Ree kwa sababu kipindi yeye anaanza kufanya muziki alikuwa pekee yake kama msanii wa kike rapper  hivyo anga zake haziwezi kufanana kabisa na anga za Rosa Ree.

Chemical anasema kuwa. ni  muda sasa kumekuwa na tabia ya mashabiki   kumfananishwa na Rosa Ree lakini swala la kufananishwa lilitkiwa liwe  ni kile  kipindi alichotoa ngoma yake kama Sielewi na VIP lakini sio sasa ambapo ameshafika mbali kimuziki tayari.

download latest music    

Sio Rosa Ree tu mimi sitaki kufananishwa na msanii yoyote, mimi nafanya muziki wangu mwenyewe.Ukitaka kufanya muziki na mimi maana yake unakuwa unaingia katika anga zangu, na ukiingia katika anga la mtu manake unakuwa tayari huwezi kwa sababu kila mtu anakuwa na namna yake ya kufanya muziki.

Nilishatoa sielewi mkaniona, nishatoa VIP mkaniona  kabla hata ya huyo rosa ree, nilitoka kipindi hiko hakuna hata female rapper bongo.

Watu wengi wamekuwa wakitaka kuwashindanisha wasanii katika game la muziki  bila kuwa na vigezo muhimu vya kuwashindanisha wasanii , hii inafanya hata muda mwingine wasanii kujenga ushindani na chuki kwa sababu ya maoni ya mashabiki wao.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.