Chegge:Nilichogundua Nitakuwa wa Mwisho Kuoa.

Chegge anaingia katika lit ya  wasanii wa zamani sana waliowahi kufanya vizuri katika kazi zao za musiki na hata sasa kuendelea kufanya vizuri pamoja na kwamba kuna ujio mpya wa wasanii chipukizi lakini wameshindwa kumkarisha chini katika game la muziki.

Tangu kipindi cha TMK mpaka sasa yeye ndie alibaki kwa kiasi kikubwa katika game na kukataa kabsa kupotea kwa sababu ya kujituma na kuheshimu kazi yake ya muziki ambayo ndio iliyompa jina na mashabiki pia.

download latest music    

Ukiachana na uzuri wa kazi zake , lakini pia Chege anaingia katika list ya wasanii wasiokuwa na skendo za mapenzi kabisa kiasi kwamba uwezi kuingia katika mtandao ukaona Chege amezungumziwa kuhusu mahusiano na msanii au mtu maarufu au yeyeote yule, hii ni kutokana na ukweli kuwa aliamua kufanya yanayohusu muziki kuwa ya muziki na mambo yake ya maisha yake kuwa na usiri sana.

akiwa katika kipindi cha Leo Tena ya Clouds Radio, akitambulisha wimbo wake mpya aliomshirikisha msanii mkongwe tanzania Saida Karoli unaojulikana kwa jina la Kaitaba, Chege alipoulizwa kuhusu mahusiano yake alisema kuwa yeye yupo katika mahusiano lakini haimaanishi kuwa kila mtu anatakiwa ajue yeye anatoka na nani.

Akiongeazea hapo Chege anasema kuwa kwa upande wake aangalii sana nani kaoa au nani hajaoa , muda wake ukifika basi na yeye ataoa lakini anahisi kuwa yeye ndie atakuwa msanii wa mwisho kuoa.

huwa sipendi kuambiwa nifanye kitu ambacho naona mwenzangu amefanya,nina mpenzi kabisa ninaempenda na tunapenda na tunaishi pamoja  muda ukifika tu mi nitaoa lakini nilichogundua mimi nitakuwa wa mwisho katika swala la kuoa.-Alifunguka Chegge.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.