“Chaz Baba Ni Wangu Hata Kama Amefunga Ndoa”- Husna Sajent
Msanii wa Bongo movie Husna Sajent ambaye amezaa na msanii wa dansi nchini Charles Gabriel ‘Chaz Baba‘ ameibuka na kudai bado anampenda baba watoto wake.
Gazeti la Ijumaa linaripoti kuwa ikiwa wiki moja imepita baada ya kufungwa kwa ndoa kisha kufuatiwa na sherehe kabambe kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar, ndoa ya Msanii wa Bendi ya The African Stars Twanga Pepeta Chaz Baba na mke wake Mariam tayari visa vimeanza.
Chaz Baba alifunga ndoa kwa mara nyingine na mwanamke aitwaye Mariam. Katika ndoa hiyo visa vimeanza baada ya mzazi mwenza wa Chaz Baba ambaye ni msanii wa Bongo Muvi, Husna Idd ‘Sajenti’ kujitokeza na kusema kuwa anachojua jamaa huyo ataoa sana, lakini mke halali aliyepangiwa na Mungu ni yeye.
Katika mazungumzo na Gazeti la Ijumaa, Sajenti alisema kuwa, Chaz Baba ni baba wa mtoto wake wa kwanza na anaamini kuwa hawezi kudumu na Mariam kwani atakuja kuwa mumewe kabisa baadaye. Sajenti alisema hata kama Chaz Baba amefunga ndoa hiyo haimpi shida kwani anajua tu atarudi kwake ili wamlee mtoto wao.
Najua Chaz ni wangu, kwani unajua zimepita ndoa ngapi kwake? Ndoa itakayodumu ni ile atakayofunga na mimi, hicho ndicho ninachokijua hadi ninaingia kaburini, asijidanganye, hawezi kudumu na huyo mwanamke (Mariam)“.