Celebtities Wanaongoza Kuwa na Maisha Magumu-Gigy Money

Mwanamuziki mwenye jina lake na drama nyingi ambae kwa sasa ametulia sana kutokana na majukumu ya uzazi ,gigy money anasema kuwa mastaa wengi ndio wanaongoza kuwa na njaa na hiyo yote inatokana na kwamba mastaa wengi wanaogopa kufanya kazi na kujipatia kipato ila wanakuwa wanategemea kupewa ela .

Maisha, unajua maisha ni magumu wala tusidanganyane siujui make-up. sijui kope,maisha hayako hivyo ni magumu tu na kuna muda watu wanaongoza kuwa na maisha magumu ni ma-celebrities.na kwa sababu yote hiyo tunaendekeza ustar mbele.mtu unajisemesha eti eeh mimi nikashike sura ya mtu nimrembe, no mimi am a gigy men, na kama nataka kufanya kitu nafanya kwa sababu sitaki kudharirika kabisa.

Gigy anaongezea kuwa katika maisha yake anaona kuwa ni bora kufanya kazi hata kama ni ngumu lakini sio kumpigia mtu simu na kuanza kumuomba ela, hata hivyo anasema kuwa kuna mambo alishawahi kuyafanya na yakamleta manufaa na hiyo inatosha hasa aliyokuwa akiyafanya hapo mwanzo kama kupiga picha za uchi.

download latest music    

Mimi nikakae nimuombe mtu mia au mia tano wakati nina nguvu ninaweza kufanya kazi,ni bora nikakuremba unanilipa elfu 50 au 60 na nikala hata siku tatu.mimi sipendi kudharirika na hakuna mtu anaeogopa kesho yake kama mimi na ndio maana  kuna vitu siwezi kufanya tena kwa sababu nilishafanya vikanifaidisha kwa nini niendelee kufanya.

Gigy money anakiri kuwa kuna baadhi ya mastaa wamekuwa wakipiga picha na kuweka katika mitandao kwa ajili ya kpata kiki na umaarufu tu na wala sio kwamba wanakuwa wana maanisha kile wanachokuwa wanajibu baada ya kitu fulani kutokea.

Niliweza kupiga mapicha ya ajabu na nimeona yamenisaidia kupata fame kirahisi na nilikuja kujua baada ya kuonamtu anakupigia simu anakulipa mtengeneze kiki.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.