Casto Dickson- Natamani Sana Kufunga Ndoa
Mtangazaji wa Clouds Tv Casto Dickson ameibuka na kuweka wazi kuwa hakuna kitu anatamani Hivi sasa kama vile kufunga ndoa.
Casto amesema ingawa anatamani kuoa lakini Mpaka sasa hajui ni mwanamke gani atakayemuoa kwa sababu kila mwanamke anayekutana naye ana sifa ambazo hazipendi.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Mchanganyiko, Casto amesema ana hamu ya kuoa, lakini tatizo linakuja kwa wanawake anaotaka kuingia nao kwenye ndoa kwani wengi wao hawako tayari na wengine kuna vitu wanavitaka hivyo mwisho wa siku inashindikana.
Unajua mimi siyo mhuni kama ambavyo watu wananifikiria, mimi ni mwanaume ninayejielewa na najua nini nafanya. Ndiyo maana huwa siruhusu hata siku moja kuyumbishwa na maneno ya mtu, kiukweli natamani sana kuoa tena ikiwezekana hata kesho ila tatizo ni kwamba bado sijapata mwanamke sahihi, wengi wao wanapenda starehe tu na siyo vitu vingine vya maana”.
Casto alikuwa kwenye mahusiano na video vixen maarufu kama Tunda Lakini aliishia kumwagwa na kuachwa na tattoo yake mkononi ambayo anayo Mpaka leo.