Calisah Amwaga Povu Zito Baada Ya Kushinda Mr. Africa
Mwanamitindo wa kiume anayeendelea kufanya vizuri katika anga za kitaifa na kimataifa Calisah Abdulhamiid amefunguka na kutoa ya moyoni baada ya kutangazwa mshindi wa shindano la Mr.Africa.
BAADA ya kufanikiwa kushinda shindano la Mr Africa International 2018, huko nchini Nigeria, Calisah ameelezea furaha aliyonayo kwa sasa na kuwashukuru Watanzania wote waliompigia kura na kuilalamikia Serikali kutompa sapoti katika safari yake ya kuelekea nchini humo.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Mara Baada ya kuibuka mshindi na kuiwakilisha vyema nchi yetu, Calisah alifunguka:
Kwa kweli nilifarijika sana baada ya kutangazwa kuwa mimi ndio mshindi, licha ya kwamba kabla ya safari yangu ya kuelekea Nigeria nilipitia changamoto nyingi ikiwemo kutopata ushirikiano kabisa toka kwa Serikali yangu, kwa sababu hata bendera niliyoitumia niliishona mwenyewe kwa fundi, hivyo nimepata tabu sana mpaka kufikia hapa”.