“Bwana Angu Anajiheshimu Siwezi Kumuanika Mitandaoni”- Queen Darleen
Msanii wa muziki wa Bongo fleva na First Lady wa WCB, Queen Darleen ameibuka na kusema kuwa kamwe hataweza kumuanika Mpenzi Wake kwenye mitandao ya kijamii kwa sababu anajiheshimu.
Kwa muda mrefu kumekuwa na masaki juu ya mahusiano binafsi ya Queen Darleen kwani ameshawahi kutoa kauli ambazo zilizua utata ikiwemo kuwa yeye hajawahi kuwa na boyfriend na ni bikra wakati ana mtoto.
Lakini Kwenye mahojiano yake na Bongo 5, Queen Darleen anaweka wazi kuwa ana Bwana lakini hawezi kumuweka kwenye mitandao ya kijamii kwa sababu jamaa huyo hapendi mambo hayo.
Simuweki wazi mwanaume wangu kwa sababu yeye mambo ya mitandao ya kijamii hapendi ni mstaarabu sana, anajiheshimu, Muislamu safi halafu ni muelewa sana kwa sababu haya mavazi yangu hana tatizo nayo kwa sababu amenikuta katika mazingira haya”.
Lakini pia Queen Darleen aliweka wazi kuwa mwanaume aliyewahi kumuweka kwenye ukurasa wake wa Instagram na kumtambulisha Kama Mpenzi Wake alikuwa ni mshkaji Wake tu.