Bongo Movies Wanaounda Kundi La Uzalendo Wamkataa Steve Nyerere
Wasanii wa bongo movies ambao wanaunda kiundi la Uzalendo Kwanza wameamua kujiweka pembeni na kuacha kukitumikia kikundi hicho na kweka pembeni kabisa harakati hizo kwa madai kuwa hawamuelewi kabisa mwenyekiti wao wa kikundi hicho Bwana Steve Nyerere ambae amekuwa akijinufaisha mwenyewe na kuacha dhana ya uzalendo kwanza.
Wasanii hao wakiongozwa na viongozi wengine kama Davina,Dude na Thea wamesema kuwa hawamuelewi mwenyekiti wao kwa sababu kila kukicha anafanya vitu kwa kutumia kundi hilo kujinufaisha yeye mwenyewe bila kujali kuwa kundi limeundwa na watu wengi na lina malengo mengi.
Viongozi hao walisema kuwa wameamua kujiweka pembeni ili kuepusha ugomvi usiokuwa na tija kwa sababu kipindi wanaanza hawakuwa na lengo baya zaidi ya kuleta uzalendo, na wanasema kuwa pamoja na kwamba wameamua kujiengua lakini bado haki zao ziko palepale kwa sababu wao pia ni waanzilishi wa kundi hilo.
Kundi la Uzalendo Kwanza lilianzishwa miaka miwili nyuma kipindi cha kampeni za uchaguzi ikiwa na lengo la kuhamasisha uzalendo kwanza kwa wananchi na kuacha maslahi ya mtu moja moja katika kuchagua viongozi wa nchi.
Steve Nyerere amekuwa akikumbwa na kashfa nyingi za kisiasa ambapo hivi karibuni alionekana hata kumkosoa kiongozi mmoja wapo mkubwa wa chama kilichopo madarakani baada ya msanii Wema Sepetu kutangaza kurudi CCM, hata hivyo kundi la uzalendo kwanza linaweza kuwa limemkataa mwenyekiti huyo kwa madai ya kile kuwa kipindi Wema anaondoka CCM kwenda CHADEMA alileta maneno maneno ya kugombana na wanakikundi hicho na kusema kuwa walikuwa wakifanya kampeni bila kulipwa ambapo wasanii wa kundi hilo walimjia juu ,ambapo aliingia ktika ugomvi na msanii mwenzie Batuli , lakini kitu cha kushangaza ni kwamba hata baada ya msanii huyo kuamua kurudi bado Steve Nyerere aliweza kumpokea .