Bongo Movie Wamwaga Povu Baada Ya Kukosa Mualiko Kwenye Harusi Ya Alikiba

Wiki iliyopita ilikuwa ni harusi ya staa wa Bongo fleva Ali Kiba na mpenzi wake Amina Khalef iliyofanyika Kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Global Publishers inaripoti kuwa Wasanii wa Bongo movie wamemjia juu Ali Kiba kwa kitendo cha kutowaalika Kwenye harusi yake.

download latest music    

GP inaendelea kudai kuwa Msanii mmoja maarufu ameibuka na kudai wameumizwa na kitendo cha kutengwa kabisa Kwenye shughuli hiyo:

Yaani harusi ilipopita, tukafanya tathimini na kuangalia idadi ya watu waliohudhuria. Tukagundua wengi ni mastaa wa Bongo Fleva, watangazaji na wadau wengine wasiohusiana na Bongo Muvi.

Kwa kweli tukagundua jamaa ni mbaguzi. Hakuwa fair, alipaswa kuwaalika angalau mastaa wachache wa Bongo Muvi kuonesha ushirikiano, mbona sisi kwenye mambo yetu huwa tunaalika watu wote?”.

Inadaiwa gazeti la Amani lilifanya uchunguzi na kugundua Kinabalu waraka ulioandikwa na wasanii hao, uliosomeka hivi:

Sisi Bongo Muvi tumekuwa tukishiriki matukio mengi ya wasanii wa Bongo Fleva iwe harusi, misiba na hata maradhi, lakini kwa tukio la AliKiba tumejiuliza sana, wasanii kama Wema Sepetu, Irene Uwoya, Jacqueline Wolper, Aunt Ezekiel, JB, Dk. Cheni, Ray, Richie, Gabo nk. ambao hata wachache chini ya hapo walifaa kualikwa.

Tulimuona Esha Buheti lakini najua yule ni mwana familia kwa upande flani, sijajua ni kipi kimetokea kiasi cha kutokualikwa sisi, lakini kwenye video zao wamekuwa wakitualika ili tupendezeshe video zao, na hata kututaja ndani ya nyimbo zao,”

Lakini pia gazeti hilo liliwahoji wasanii kadhaa ili kupata mtazamo wao juu ya hilo na waliongea haya:

Aunt: Nisingependa kabisa kuongelea kuhusu hilo.

Wolper: Kwa kweli sikupewa mualiko lakini pia nilikuwa naumwa.

Steve Nyerere: Siwezi kulalamikia kutoalikwa kwenye harusi japo najua hayo mambo ya utimu yanaweza kuingia.

Ali Kiba alipotafutwa kwa ajili ya kujibu tuhuma hizo hakuweza kupatikana.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.