Bond Azungumzia Swala la Matibabu ya Wastara.
Msanii wa bongo movie nchini Bond bin Sina , amefunguka na kutoa maoni yake juu ya taarifa za matibabu ya Wastara na kwanini msanii huyo ameamua kuomba msaada wakati anao ndugu zake .Bond anasema kuwa Wastara ameomba msaada kwa wananchi kwa sababu ametapa shida sana na ni kweli kuwa kwa wakati huu anahuitaji hivyio watu wajitolee kumsaidia.
Wastara ambae hivi karibuni alifunguka na kulalamika kuhusu matibabu yake ya mwanzo amabyo alikuwa akipatiwa nchini india kwa usaidizi wa mume wake , wastara alilalamika na kusema kuwa mwanaume huyto alimnyanyasa sana baada ya kutoka hospitali kwa kumdai risiti za matibabu na kusema kuwa alikuwa akijisikia vibaya na kuona kama vile alikuwa akinyanyaswa na shida za ugonjwa wake.
Bond anasema kuwa swala la Sadifa kuomba risiti ilikuwa sawa kwa sababu yule ni mbunge na matibabu yake yanalipiwa na serikali hivyo kuonyesha risiti ilikuwa ni kutaka kujua ni kiasi gani kinapaswa kulipwa.
kuhusu risti hayo ni makosa yake mwenyewe kwa sababu unapoachana na mtu haupaswi kuongea kila kitu kuhusu yeye.kuhusu kuomba risti baada ya kutoka katika matibabu ilikuwa ni sawa kwa sadifa kwa sababu yeye zile pesa anarudishiwa na serikali so haikuwa kosa kumuuliza kwa sababu wale walishafanyiana vitu vingi ila yeye kaongea ili sadifa aonekane mbaya.
Bond alikuwa mpenzi wa wastara baada ya Wastara kufiwa na mume wake wa kwanza sajuki, lakini walikuja kuachana na sababu kubwa ya kuachana kwao bond anasema kuwa wastara amekuwa ni mwanamke anaehitaji ela na mafanikio ya haraka bila kuangaika na ndio maana walishindwana.hata hivyo kipindi Bond anapata matatizo na kuwekwa selo wastara hakusumbuka hata siku moja kumjulia hali au kusaidia kufanya kitu chochote.
Bond anamaliza kwa kusema kuwa kipindi yuko na wastara alikuwa akimsaidia na kumuweka sawa kwa vitu vingi sana.
Kipindi mimi niko nae nilikuwa namuweka sawa vitu vingi sana kwaio kwa sasa inategemea mwanaume gani alienae kama anamzidi akili basi vitatokea vitu vingi sana.