Black Pass Apata Kigugumizi Kufanya Kazi na Ebitoke.
Msanii wa vichekesho maarufu kama Black Pass ambae amepata umaarufu mkubwa kutokana na kuigiza kwake akiwa kama kiziwi na bubu amepata kigugumizi kujibu swali alilokuwa ameuliza na watangazaji wa Times Fm kuhusu yeye kumjua ebitoke na kama anaweza kufanya nae kazi ya vichekesho kwa sababu wote wapo katika tasnia moja.
Black Pass ambae alionekana kuwa na kigugumizi huku akijifanya ajaelewa swala aliloulizwa baadae alijibu na kusema kuwa anaweza kufanya nae kazi lakini kwanza ni lazima apewe ruhusa kutoka kwa uongozi wake anaofanya kazi.
Mimi nafanya kazi na kampuni na kama kampuni itaniruhusu mimi nafanya kazi na mtu yoyote na ikitokea kama uongozi unakubali na kuniambia nifanye nae kazi mimi nitafanya.
Ebitoke na Black Pass wamekuwa wakifananishwa na kushindanishwa sana katika mitandao ya kijamii kwa sababu ya kazi zao , huku wengine wakisema kuwa Ebitoke ameshushwaa kiwango kutokana na uwepo wa mwanadada huyo ambae ana kipaji kikubwa katika vichekesho kuliko Ebitoke.