Bilnass kufanya kolabo na alikiba
Msanii anaetamba kwa sasa na wimbo wake mpya wa funga geti BILNASS amefunguka na kusema kuwa ile kolabo aliokuwa akisubiri kuifanya kwa muda mrefu kati yake na Alikiba kwa sasa imekwisha kamilika na iko mbioni kutoka.
Akiongea na Times Fm , Billnass anasema kuwa wimbo huo uko tayari lakini hawezi kuutoa kwa sababu ya Alikiba yuko chini ya uongozi ambao ni lazima kufuata utaratibu fulani kabla ya kuachia ngoma , hivyo taratibu hizo zikikamilika basi wataweza kuutoa.
kolabo na Alikiba tayari tulishafanya bado tu kutoka kwa sababu ya taratibu zao na hii ni kwa sababu alikiba yuko chini ya Sony na wamekuwa na utaratbu wao, Hivyi ninasubiria utaratibu wao tu kama itatoka mwakani au mwaka huu.