Billnass Afurahia Petit Man kuondoka LFLG
Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchi Billnass amesema kuwa kuondoka kwa aliyekuwa meneja wake wa zamani Petit Man kumempa unafuu kidogo ukizingatia kuwa kuna vitu alivyovifanya meneja huyo ambayo vilileta athari kubwa saa kwake kuliko kwa mtu mwingine yoyote katika lebo yao ya lflg.
Akiogea leo katika XXL ya Cloud Tv, wakati akitambulisha wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Tagi ubavu (self made) , Billnass anasema kuwa Petit Man aliamua kuondoka siku zzi nyuma kidogo lakini haweiz kusema chochote kuhusu kuondoka kwake kwa sababu hata wakati anaingia na kupokelewa hakuna aliyejua wala hakuna aliesema kwanini aliingia katika lebo hiyo.
Siwezi kusema kwanini ameondoka kwa sababu hata wakati anaingi hakuna aliyesema kwanini ameingia.Kuondoka kwake hakujaniathiri chochote kwa sababu hata wakati yupo kuna kitu alikifanya na kiliniletea damage kubwa sana kwa upande wnagu kuliko kwa mtu yoyote,kwaio imekuwa sawa maana ni kama vile nilikuwa namsubiri aondoke tu.
Hata hivyo billnass alipoulizwa kuhusu uhusiano wao kwa sasa na kwanini anaonekana kama anafurahia kuondoka kwa aliyekuwa meneja wake petit, bill nass alisema hawajagombana na wako poa kabisa.
Mimi na Petit tunaongea poa tu na tunawasiliana hatujagombana kabisa ila tu hatuko pamoja tena kama zamani.
Bilnass na Petit Man walikuwa ni watu wanaofanya kazi pamoja na hata baadhi ya sehemu walikiwa wakionekana pamoja kama meneja na msanii wake hata baadhi ya ngoma za bill nass kama ile ya chafu pozi na petit man alionekana akitokea katika video hiyo.mpaka sasa hakuna aliye tayari kati yao kuweka bayana ni kitu gani kimewatenganisha au ni damage gani aliingiza kwa Billnass.
Bilnass ametoa wimbo mpya na ameufanya chini ya producer na menaja T-Touch