Billnas Afunguka Sababu Za Kumpotezea Nandy
Msanii wa Hip hop nchini William Lyimo maarufu kama BillNas amefunguka na kuweka wazi sababu zilizopelekea kumpotezea aliyekuwa Mpenzi Wake Faustina Charles ‘Nandy’ wikiend iliyopita.
Wikiendi iliyopita Msanii Nandy alifanya uzinduzi rasmi wa albamu yake ya ‘The African Princess’ na katika hafla hiyo Billnas alikuwepo ndipo Nandy alipomfuata Billnas kwa ajili ya kuimba wote lakini cha ajabu Billnas alimpotezea kabisa Nandy.
Baada ya sakata hilo BillNas amefunguka Kwenye mahojiano na kipindi cha Enews na kusema sio kila sehemu anaenda Kama msanii kuna sehemu nyingi anaenda Kama mtu wa kawaida tu na anakuwa hayuko tayari kuimba na haikuwa lazima kushiriki kama msanii.
Sapoti niliyotoa ya kununua albamu na kufika pale ilitosha, sioni sababu ya kuendeleza uadui kati yangu Mimi na Nandy Mimi nilienda pale kumpa sapoti yangu ya kweli kama msanii mwenzangu na si vinginevyo, hivyo alivyonipa mic sikujuwa nifanye nini kwa muda ule kwa kuwa sikuwa tayari kuimba kabisa”.
Lakini pia Billnas amefunguka kuwa ni miezi Sita imepita tangu atoe nyimbo yake hivyo amewataka mashabiki wake wakae mkao wa kula kwani muda wowote anaachia mambo.