Biashara Zangu Ndio Zinanikondesha Sio Kingine-FaIza Ally
Muigizaji wa Bongo movie na mzazi mwenza kwa Mbunge wa Mbeya Mjini Sugu, Faiza Ally amefunguka na kuweka wazi kuwa kinachomkondesha kwa hivi sasa ni biashara zake.
Faiza ambaye amesuka gumzo baada ya kuonekana anapukutika mwili wake amedai kuwa anakonda kutokana na mizigo ya watu kuchelewa kufika kwa wakati.
Kwenye mahojiano yake na gazeti la Ijumaa Wikienda, Faiza amesema kuwa watu wengi wanamzungumzia na kumshangaa jinsi alivyopungua, lakini hawajui ni jinsi gani hali wala halali usiku kwa sababu ya mizigo ya watu kuchelewa kufika bandarini.
Watu wengi wananiuliza ninakondeshwa na nini, lakini hawajui ni jinsi gani ninakosa amani mizigo ya watu walioniagiza isipofika kwa wakati ninachanganyikiwa kabisa”.
Faiza ni mmoja kati ya wajasiriamali wa Kwenye Instagram ambaye anafanya biashara ya Kukutwa watu vitu kutoka China kuja Tanzania.