Ben Pol- Muziki Wa RnB Unahitaji Uvumilivu Ili Kupata Mafanikio
Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayetamba kwa miondoko ya muziki wake wa RnB Bernard Paul maarufu kama Ben Pol amekiri muziki huo haulipi na unahitaji uvumilivu.
Ben Pol ambaye ameshawahi kutengeneza hits songs kibao kwa miondoko yake ya RnB amekiri kuwa muziki aina hiyo ya muziki kutusua sio rahisi na kukiri msanii anahitaji uvumilivu wa hali ya juu ili kupata mafanikio.
Kwenye mahojiano na Kipindi cha The Dj Show cha Radio One, Ben Pol amefunguka haya:
RnB ni muziki ambao unahitaji mtu uwe na passion kwa sababu asilimia kubwa ya miziki ya RnB haifanyi biashara vizuri, haiuzi . Kwa hiyo wale wachache wanaofanya kwa moyo na kubadilisha kidogo na kuifanya Kitanzania, wanaimba kiswahili fasafa, unaona kina Jux, Rama Dee, Ben Pol wanaweza kufanikiwa kuwafikia watu.
Lakini wengine wanaingia kwa mkumbo kwa kujaribu ndio wanashindwa wanaingia kwenye miziki mingine ambayo ndio inaonekana unauza hapo hapo, hata hao wengine inadoda pia”.