Ben Braker Amzungumzia Brown, Asema Haeleweki.
Model wa kiume bongo Ben ambae amekuwa akitokea katika video mbalimbali na huku akifanya kazi zake za mitindo amemzungumzaia model mwenzake Brown,ambae aliweza kupata kiki sana kipindi anatoka kimapenzi na msanii mkubwa bongo Wolper Jackline.
Ben amesema kuwa brown anashindwa kueleweka ni kitu gani amekuwa akifanya mjiki kwa sababu anafanya vitu vinavyomchafua katika jamii mpaka kumfanya kumharibia kazi zake.
Ben anasema kuwa kipindi cha kwanza mwenzake huyo alikuwa akifanya vizuri lakini alipoanza kutembea na watu wanaomzidi umri na kukaa ndani ndipo alipoanza kufulia na watu kumdharau na kumwita kiben ten na kwamba hana ela mjini.
mara ya mwisho miaka ya 2015 Brown alikuwa akifanya fashion shoo lakini baadae nikaona Brown kama haeleweki anafanya nini,ndo anajikuta sasa anaanza kutoka na wasanii wa bongo movies mara kajipiga tatoo ya nani sijui, najua zile pia ni kiki zinakufanya ujulikana lakini mwisho wa siku unapomwambia mtu kuwa wewe ni mdoel akikwambia uweke profile yako kwamba hakujui , kuna watu ni professional model na wengine ni model jina tu.Na ndio maana sasa hivi watu wanamwita kiben ten—Alifunguka Ben Blaker laipokuwa akiongea na bongo5
Brown alijiingiza katika mahusiano na wolper na kupata umaarufu sana lakini baadae alikuja kushindwana na wolper na sasa yuko katika mahusianona Nisha.Kutokana na tabia yake ya kupenda kulelewa , brown amekuwa akidhaurika sana katika mitandao ya kijamii.