BAVICHA Wamtaka Naibu Waziri Kutengua Kauli ya Kumfungia Roma.
Baraza la Vijana Chadema wamemtaka Naibu Waziri Habari, Utamaduni na Michezo kutengua kauli yake ya kumfungia msanii wa muziki wa kizazi kipya Roma Mkatoliki kwa kuwa sio jukumu lake kumfungia msanii huyo au msaniii yoyote.
BAVICHA wamedai kuwa jukumu la kuwafungia wasani linatoka kwa BASATA hivyo wameshangazwa na kitendo cha Mh Juliana Shonza kuingilia kati swala hilo na kutangaza kufanya maamuzi hayo yeye kama yeye kwa sababu hakupaswa kutangaza.
Serikali hii haioni kuwa kuna kila sababu kwa sababu hali ya uchumi ni mbaya , lakini leo unamsimamisha msanii asifanye kazi ambayo anaitegemea kwa miezi sita , kwanza sheri haimoi mamlaka Waziri , mamlaka hiyo ameitoa wapi waziri?
mamlaka hiyo ipo kwa BASATA yeye kazi yake ni kuisimamia BASATA tu aielekeze BASATA wafanye kazi gani na sio yeye Naibu Waziri, Sisi kama baraza tunaona kama naibu waziri kwakweli amepotoka.Naibu Waziri amekosea na tumesikitishwa sana na tuna kila sababu ya kusema kuwa tunakemea.Serikali na Waziri mwenye zamana hiyo wanapaswa kutengua maamuzi hayo na wale waliochelewa mpaka nyimbo hizo zikapigwa zaidi ya mwaka mmoja wanapaswa kupewa adhabu pia.
Lakini pia BAVICHA wamewataka BARAZA na naibu waziri kutokufanya kazi kwa kushinikizwa na watu binafsi.H hata hivyo msemaji huyo wa BAVICHA Bwana Sosopi amesema kuwa hakuna mtanzania anaetaka kuvunjwa kwa maadili lakini inabidi BASATA watoe hukumu pale panapostahili.
Mpaka sasa Roma hajajitokeza kuongelea swala hilo ingawa kumekuwa na watu wengi nyuma yake wakimsapoti, lakini inasemekana kuwa msanii huyo kwa sasa yupo nje ya nchi kikazi.