Batuli Awachana Wasanii Wa Kike Wanaoharibu Sanaa.

Msanii wa bongo movie Neshy Adam maarufu kama Batuli amefunguka na kuwabwatukia wasanii wa kike wanaoingia katika sanaa na kujifanya wao kuwa ni wasanii kumbe lengo lao ni kuharibu sana  ya bongo.Batuli anaonekana kukwera na tabia za mabinti wenzie ambao wamekuja na kuingia katika sana na kuanza kutafuta kiki zisizokuwa na msingi huku  wakiharibu heshima ya sanaa nchini.

Batuli anasema kuwa wasanii wengi ambao wa wamekuwa wakitupia picha za uchi katika mitandoa wakichunguzwa vizuri unakuta hawapo katika kundi lolote sio la muziki wala filamu na hata majina yao wameyapata kwa kutengeneza kiki za kupiga picha za uchi.Hata hivyo Batuli anawaomba sana wasanii hawa waiheshimu sanaa kwa sababu wameikuta haijachafuka.

download latest music    

Asilimia kubwa ya wanaotupia picha chafu katika mtandao hawapo katika makundi haya mawili  la muziki wala filamu.umaarufu wao wameupata  kwa kupiga picha za uchi na kuzitupia katika mitandao  ya kijamii, na watanzania wasiokuwa na maadili kuwapokea kwa shangwe.#sanaaipeweheshimayake.

maneno ya Batuli yamemtoka baada ya ku-trend kwa habari ya naibu waziri kuanza kutoa adhabu kwa wasanii wote wakike ambao wanapiga picha za uchi na kuzichapisha katika mitandao ya kijamii ambapo ameanza na Gigy Money,Sanchi na Pretty Kindy ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mh .Raisi la kuimarisha maadili ambayo yamekuwa yakivunjwa na watu wa aina hiyo.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.