BASATA Wakanusha Kukwamisha Mashindano ya Miss Tanzania.

Wiki uliyopita kampuni ya LINO entertainment walitangaza kushindwa kufanikisha fainali za mashindano ya Miss Tanzania kwa mwaka huu huku ikisema kuwa moja ya vitu vilivyokwamisha mashindano hayo  ni BASATA ambao walichelewa kuwapa kibali kampuni hiyo hivyo kufanya kushindwa kutafuta wadhamini kwa muda muafaka.

Siku ya jana BASATA walitoa tamko lao na kukanusha taarifa hizo zilizosemwa na LINO Entertainment kuwa wao ni moja ya sababu ya kukwama kwa shindano hilo.

download latest music    

BASATA wamesema LINO kutamka kuwa waondio wamesababisha tatizo ilo ni uongo inawzekana ilikuwa ni kuficha matatizo yao mengine lakini sio kweli kuwa wao ndio chanzo.

mashindano ya  Miss Tanzania mwaka huu yameshindwa kufanyika kutokana ma kukosekana kwa udhamini wa mashindano hayo , sababu ambayo imeletwa baada ya kucheleweshwa kwa kibali cha kufanya shindano hilo.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.