BASATA na Waziri Wake Wanatafuta Kiki:-Belle 9
Kumekuwa na wimbi la wasanii na wadau mbalimbali wa muziki wakijaribu kutoa maoni yao kuhusu swala la naibu wa ziri mh juliana shonza kufungiwa wasanii wa muziki wa bongo nyimbo zao kwa madai ya kuwa nyimbo hizo hazina maadili.
Msanii Belle 9 nae pia ameibuka na kuongelea swala hilo na kusema kuwa kitendo hicho kwa mara ya kwanza alpokisia hakuchukulia kama jambo baya lakini kwa jinsi siku zinavyoenda na kuona hali inavyokuwa amegundua kuwa naibu waziri na BASATA wanatafuta kiki kupitia wasanii.
Naibu waziri ambae hivi karibuni aliongea na waandishi wa habari juu ya swla hilo, alikuwa akishindwa kujibu baadhi ya maswali ya msingi kutoka kwa wadau wa muziki kitu kilichowafanya watu na wasanii waone kuwa naibu waziri hana sababu ya msingi ya kufanya hivyo.