Barakah The Prince Afunguka Kuhusu Kumwagana na Naj na Mpango Wa Kutoa Nyimbo Mpya Kila Wiki
Mwanamuziki wa Bongo fleva wa kujiita Magufuli wa Bongo fleva, Barakah the Prince amefunguka kuhusu tetesi za yeye kumwagana na mpenzi wake na mwanamuziki mwenzake, Naj na pia afafanua mpango wake wa kuwa anatoa nyimbo mpya kila baada ya wiki moja.
Barakah anayetamba na wimbo wake mpya wa ‘Sometimes’ amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na Naj kwa kipindi kirefu sasa ambapo siku za nyuma walikuwa ni kawaida yao kuposti picha mtandaoni wakiwa pamoja au kila mmoja kumposti mwenziye lakini ghafla taratibu hiyo ikapotea na ndipo wengi walidhani kuwa watakuwa wamemwagana.
Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo cha televisheni cha East Africa, Barakah alifunguka yafuatayo kuhusiana na ishu hizo:
Napenda kuwaambia mashabiki zangu kuwa wimbo wangu wa ‘sometimes’ ndio wimbo wa kiwango cha chini katika listi ya nyimbo nitakazotoa ambazo ntaanza kutoa kila wiki, yaani kila wiki ntakuwa naachia ngoma mpya kwa sababu mashabiki zetu tunakuwa tunawaangusha kwasababu wanataka kila siku wawe wanasikiliza nyimbo mpya alafu pia nyimbo zikiwa nyingi inatupa changamoto wasanii ya kufanya kazi nzuri zaidi, unajua zamani nilikuwa naweza kutoa nyimbo moja kwa miezi sita sahivi nabadilisha utaratibu kwa sababu mashabiki wamebadilika na mziki ni biashara kwaiyo inabidi niangalie wateja wangu”.
Barakah pia aliongelea uhusiano wake na Naj:
Sasa mimi nasapotije kazi yake ya mziki wakati na yeye ni mwanamuziki anahitaji yeye mwenyewe kupromote kazi yake, kwanza kazi na mapenzi haviwezi kuingiliana hata siku moja nilimsapoti kwa kazi yake ilipoishia ndo hapo hapo kwani ile ni page yangu mimi mwenyewe nataka kuposti vitu vingine mbali na Naj, tukiwa Nyumbani tunaonyeshana mapenzi sio lazima tuonyeshane Instagram, lakini hajanimwaga Mimi nikimwagwa kila mtu atajua kwasababu ukinimwaga nataka uwe adui yangu mi sijaachana na Naj tungekuwa tumeachana Mimi ningesema yule sio mpenzi wangu lakini bado tuko wote ila kwa sasa yupo nyumbani kwao London”.