Banana Zoro Amjibu Shabiki Aliyesema Amefulia
Mwanamuziki mkongwe alianza muziki zaidi ya miaka 10 iliyopita huku akiwa chini ya baba yake Mzee Zahiri Ally Zorro ambapo ilikuwa ikijulikana kama familia yenye vipaji kwa sababu kwao wote walikuwa wasanii Banana Zoro , amefunguka katika kipindi cha eNews cha East Africa Tv na kujibu tuhuma zinazomkabili za kufulia na kwa sasa amnapumulia mipira.
katika vipindi vinavyondeshwa na EATV, mashabiki walipewa nafasi ya kuzungumzia hali za wasanii mbalimbali ndipo shabiki mmoja aliposema kuwa Banana Zoro amekuwa kimya na kuwa amefulia ndio maana yupo kimya, hata hivyo Banana alipopata nafasi ya kujibu tuhuma hizo alisema kuwa mashabiki hawapaswi kukariri maisha ya wasani kwa kuwa wengi wamezoea kuonyesha maisha yao katika mitandao kwa sababu kwa upande wake hajazoea kufanya maonyesho katika vyombo vya habari kuhusu maisha yake lakini yuko viuzri sana.
Mafanikio ni wewe na dreams zako wakati unakuwa ulitaka kuwa na nini,uwezi kusema sijafanikiwa wakati haunijui kiundani, na mimi siwezi ku-display kila kitu changu katika mitandao, lakini am gud, i have my wife, my kids, my band na mimi ndio msanii wa kwanza kuwa na band yangu mwenyewe Tanzania na inafanya vizuri.Na pia nimeajiri watu katika bandi yangu zaidi ya 20 ,nafikiri hayo ni mafanikio makubwa sana.
Hata hivyo Babana Zoro anasema kuwa ni kweli kuna baadhi ya wasanii wakubwa na walikuwa wanafanya kazi vizuri kabisa lakini ukiangalia maisha yao kwa sasa yanatia aibu kabisa na hawajiwezi kwa lolote lakini kwa upande wake ni tofauti kwa sababu anausafiri wake na ana nyumba yake na anaendesha maisha vizuri kabisa.
ukisema mafanikio kwa sasa labda tunapigana ili kujulikana kimataifa zaidi,lakini mimi nimenunu agari nina miaka 18 mapaka sasa nina miaka 36 na hata hivyo siwezi kusema nina gari gani kwa sasa kwa sababu at the end of the day gari langu ni gari langu, sikimbizani na daladala tena ingawa kuna wasanii mpaka leo walikuwa wakubwa lakini bado wapo huko na wana hali mbaya .Sisemi kuwa kupanda daladala ni vibaya.naishi kama nyumba yangu iko maramba mawili na its one of the best houses.