Bajeti ya Birthday ya Uwoya Inatisha :-Steve Nyerere
Msanii wa maigizo ya bongo movies Steve Nyerere ambae mara zote amekuwa kama kiongozi kwa wasanii wengine amefunguka na kusema kuwa bajeti ya sikukuu ya kumbukumbu ya kuzaliwa ya mwanadada Irene Uwoya ni zaidi ya mamilioni ya pesa na wala haina haja ya kuitamka hadharani.
Mwanadada irene ambae ametimiza miaka 30 hivi karibuni allifanya sherehe hiyo huku akitoa msaada kwa watoto wenye uhitaji na pia kupokea zawadi mbalimbali kwa watu wanaompenda inasemekana kuwa amefanya shughuli hiyo kwa pesa nyingi sana.
Steve Nyerere anasema “bajeti ya birthday ya irene imevunja rekodi ni zaidi ya najeti ya wizara na ninaomba tusiiseme hadharani atatafutwa na TRA.”