Baby J Atangaza Mapinduzi Kwenye Bongo Fleva
Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka katika visiwa wa Zanzibar Jamilah Abdullah maarufu kama Babu J ametangaza kufanya mapinduzi makubwa pindi atakaporudi kwenye Sanaa.
Baby J ambaye ameshawahi kutengeza nyimbo kali katika kipindi cha nyuma amekuwa kimya sana katika miaka ya karibuni.
Baby J amevunja ukimya Wake na kuweka wazi kuwa kwa sasa yupo mafichoni lakini Ana mpango wa kuibuka tena na anaamini endapo atarudi atafanya mapinduzi makubwa.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Baby J alisema kuwa ni kweli yuko kimya lakini kuna vitu anavipanga akimaliza ataibuka na kuwa vizuri kabisa.
Najua watu wengi wanajiuliza nipo wapi lakini nashukuru sana Mungu nilipojificha ni kwa ajili ya mambo mazuri na si vinginevyo”.