Baba Mzazi wa Ali Kiba Azikwa Katika Makaburi ya Kisutu
Baba mzazi wa msanii ali kiba pamoja na Abdul Kiba amezikwa mchana wa Janauary 17 katika makaburi ya kisuu jijini dar es salaam.
Mauti ya mzee saleh yalimkuta alfajiri ya January 16 katika hospitali ya Muhimbili alipokuwa anapatiwa matibabu yake , ambapo moja ya wasemaji wa familia abdul kiba alisema kuwa baba yake alipatwa na malazi ya kupalalaizi wiki mbili zilizopita ambapo ugonjwa huo uliathiri sana sehemu za ubongo.
Umati wa watu umejitokeza kwa ajili ya kufanya mazishi ya baba mzazi wa wasanii wao mpendwa pamoa ana wasanii mbalimbali walionekana kuguswa na tukio hilo.
Alikiba, Abdul kiba na ndugu wengine wakichukua mwili wa baba yao mzazi hosptali ya Muhimbili
Mwili wa marehemu ulipokuwa unawasili nyumbani kwake kariakoo.
Mwili wa marehemu ulipokuwa unapumzishwa katika makaburi ya kisutu.