Baba Levo Awekwa Huru na Mahakama
Msanii wa Bongo fleva na diwani wa kata ya Mwanga Kaskazini Kupitia Chama cha ACT Wazalendo Crayton Chipando maarufu kama Baba Levo ameachiwa huru na mahakama.
Baba Levo ambaye aliingia katika upande mbaya wa sheria mwezi uliopita baada ya kudaiwa kumfanyia vurugu Muuguzi.
Baba Levo alikuwa akikabiliwa na mashtaka matatu ya kushambulia, kufanya vurugu na lugha ya matusi dhidi ya muuguzi, Christina Gervas wa Zahanati ya Msufini.