Baba Diamond: Sijawahi Kuongea na Zari Ila Hamisa na Wema Nimeshaongea Nao
Baba mzazi wa Mwanamuziki Diamond Platnumz, Mzee Abdul Juma amefunguka kuhusiana na uhusiano wake na mkwe wake Zari na kukiti kuwa hajawahi kuonana naye wala kuongea naye ila ameshaongea na Wema pamoja na Hamisa.
Sio siri kuwa Diamond na Baba yake Mzee Abdul hawana uhusiano mzuri sana miaka michache iliyopita Baba wa Diamond alienda kwenye vyombo vya habari na kutangaza kuwa mwanaye Diamond hamjali kwa chochote kile na amemtupa, Diamond aliweka wazi kuwa baba yake alimkataa tangu akiwa mdogo na ni mama yake pekee ndiye aliyemlea.
Tangu hapo Diamond na baba take wamekuwa wakiongea vitu viwili tofauti na vyombo vya habari. Baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu Baba Diamond alirudi kwenye vichwa vya habari miezi michache iliyopita baada ya kushiriki kwenye Arobaini ya mtoto wa Hamisa ambayo mwanaye Diamond na familia yake hawakuudhuria.
Baba Diamond alipofanya mahojiano na Millard Ayo alifunguka mengi kuhusu wajukuu zake na mkwe wake Zari:
Nikitaka kuwasiliana na wajukuu zangu walio nchi za nje naonana na Mama Nasibu nampa salami tu basi lakini nikitaka kuonana na mjukuu wangu mtoto wa Hamisa kwa kuwa yupo hapa Dar karibu na ninapoishi hivyo wanakuja tu kunichukua basi lakini kusema kweli Zari sijawahi kuzungumza naye ila katika wakwe zangu mtu wa kwanza kuzungumza naye alikuwa Wema Sepetu na Hamisa Mobetto ambaye kusema kweli namshukuru kwa kunipa heshima zote Kama babu kwa kumpa mjukuu wangu jina langu kwa kweli namshukuru Sana”.